RONALDO ATANGAZA VITA YA BALLON D'OR KWA MESSI, NEYMAR NA LEWANDOWSKI

STRAIKA  Cristiano Ronaldo amewatangazia vita mastaa wenzake, Lionel Messi, Neymar na Robert  Lewandowski baada ya kusema kwamba  ndio atahakikisha anapambana nao vilivyo  katika vita ya kuwania tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Ballon d'Or kwa mwaka huu.

Staa huyo alitangaza vita hiyo juzi na alisema kwamba, wakati akijiandaa na msimu ujao mahasimu wake watakuwa ni nyota hao watatu na ushindani wao kwake ndio utakaomsukuma afanye makubwa zaidi.

Kinara huyo ambaye ndiye anayeishikilia tuzo hiyo ya Ballon d'Or, alisema licha ya kuwa kuna kazi kubwa kwake ya kuifanya ili kuitetea, lakini akasema anavyoamini kiwango kitakachooneshwa na wapinzani wake hao msimu ujao ndicho kitakachomfanya ainyakue kirahisi.

“Bila shaka mara zote huwa ni vita kati yetu,” staa huyo aliuambia mtandao wa  ESPN hivi karibuni wakati akiwa ziarani nchini China.

"Kwa muda mrefu nimekuwa katika vita hiyo na Lionel Messi, Neymar, Robert  Lewandowski na Gonzalo Higuain,” aliongeza staa huyo.

"Vita ya aina hii mara zote huwa ni kubwa na yenye ushindani na hicho ndicho hunifanya niwe bora zaidi kuliko wao mwaka hadi mwaka,” alikwenda mbali zaidi nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Ureno.

Alisema kwamba, ukiwa bora ni lazima ujaribu kushindana na walio bora ili uweze kuendelea kuwa bora na huku  akisisitiza kuwa daima usipoteze malengo kwa kile alichodai ni washindani wako wanaweza kukupita.

No comments