RONALDO NAYE AMZUIA NEYMAR KUONDOKA BARCELONA

BAADA  mastaa Lionel Messi na Luiz Suarez kumweka chini mwenzao, Neymar asiondoke Barcelona, nyota kadhaa wamezidi kujitokeza ili kumsihi asiondoke.

Safari hii aliyejitokeza ili  kumpa darasa straika huyo ni Cristiano Ronaldo ambaye amemtaka Mbrazil huyo kutokubali kuhama kwa ada hiyo itakayovunja rekodi ya usajili dunia kwa kwenda kujiunga na  Paris Saint-Germain.

Ronaldo alisema jana kwamba tayari ameshampigia simu staa huyo wa timu mahasimu wao, Barcelona akimueleza kuwa atakuwa amefanya makosa makubwa endapo ataamua kwenda kucheza soka nchini Ufaransa.

Mbali na hilo, staa huyo wa  Real Madrid  alisema pia katika mazungumzo yao hayo alimshauri Mbarazil huyo akajiungea na  Manchester United endapo ana dhamira ya dhati ya kuitosa klabu hiyo ya  Nou Camp.

Inaelezwa kwamba nyota huyo wa Real Madrid, Ronaldo na  Neymar  wana urafiki wa karibu sana licha ya kuwawanachezea timu pinzani na uhusiano huo ulikua zaidi wakati wawili hao wakiwa chini ya udhamni wa Kampuni ya  Nike  na jarida moja  la michezo nchini Hispania, Diariogol liliripoti kuwa nyota hao wamekuwa wakipigiana simu ili kujadili dau hilo la pauni milioni 192 alilotangaziwa  Neymar ili akajiunge na  PSG.


Jarida hilo lilieleza kuwa  katika majadiliano hayo, Ronaldo  amekuwa akituma ujumbe mara lkadhaa kupitia mtandao wake wa  WhatsApp  akimuonya staa huyo mwenye umri wa miaka  25 asiondoke kwenye michuano ya  La Liga na kwenda kujiunga  Ligue 1 kwa  kile anachodai atakuwa amepoteza mwelekeo.

No comments