"RONALDO NI WA HAPAHAPA REAL MADRID" ZIDANE AWATHIBITISHIA MASHABIKI WAO

PAMOJA na changamoto mbalimbali anazokutana nazo kimaisha katika klabu yake ya Real Madrid, lakini mshambuliaji nyota wa timu hiyo, Cristiano Ronaldo hataondoka.

Kocha wa timu hiyo, Zinedine Zidane amesema kwamba anajua kila kinachomsibu Cristiano Ronaldo lakini anadhani kwamba hayo ni matokeo ya kuwa mchezaji mkubwa.

“Sidhani kama kuna haja ya kuwa na wasiwasi najua kwamba Ronaldo ana mitihani mingi lakini najua kwamba hataondoka kokote katika wakati huu,”amesema kocha huyo.

Amesema kwamba Ronaldo ni mchezaji wa kiwango cha juu mwenye uwezo mkubwa ni tunu pekee kwa Real Madrid.

“Sidhani kama kuna haja ya kuwa na wasiwasi. Najua kwamba Ronaldo ana mitihani mingi lakini najua kwamba hataondoka kokote katika wakati huu,” amesema kocha huyo.

Amesema kwamba Ronaldo ni mchezaji wa kiwango cha juu mwenye uwezo mkubwa na ni tunu pekee kwa Real Madrid.

Kumekuwa na habari kuwa mchezaji huyo anataka kuondoka katika kikosi hicho kutokana na misukusuko ya kodi anayokutana nayo kwenye taifa la Hisnania.

Kumekuwa na habari kwamba mchezaji huyo anawindwa na PSG pamoja na Man United ambako alikuwa anacheza kabla ya kujiunga na Real Madrid.

“Pamoja na kwamba kuna matamanio ya timu nyingine kwamba wanamtaka baada ya kusikia kwamba ana matatizo hapa lakini dhahiri kwamba anaendelea kuipenda Madrid.”

Akihojiwa na kituo cha michozo cha Sport Talks Zidane amesema kwamba Ronaldo ataendelea kuwa katika kikosi cha Real Madrid misimu ujao.


“Nimeongea naye na amesema naye hana matatizo na timu. Msiwe na wasiwasi Ronaldo ni wa Real Madrid na ataendelea kuwa nasi.,” amesema.

No comments