SAHIHI YA JAMES RODRIGUEZ SASA YAFIKIA PATAMU ...Man United yapigwa za uso, Bayern Munich vijogoo


CARLO ANCELOTTI amefanikiwa  kumpeleka Bayern Munich straika wa Real Madrid, James Rodriguez na kuiacha kwenye mataa Manchester United iliyokuwa ikimsaka nyota huyo kwa udi na uvumba.

Rodriguez, mchezaji aliyefunga mabao 17 na kupika 18 katika mechi 46 alizocheza kwenye La Liga, anakwenda Bayern kwa mkopo wa miaka miwili.

Bayern Munich pia imewekewa kipengele cha kumnunua jumla mchezaji huyo baada ya Juni, 30 mwaka 2019. 


No comments