SAID NDEMLA ANUKIA AFC YA SWEDEN... Simba sasa yampa baraka zote

KIUNGO mwenye utundu mwingi uwanjani, Said Hamis Ndemla wa Simba ni kama ameshaanza kuagana na soka la Tanzania kufuatia habari kwamba wakati wowote anaondoka nchini.

Habari kutoka Simba zinasema kwamba Ndemla anaondoka wakati wowote kuanzia sasa kwenda kujiunga na klabu ya Athletic Footbal Club Eskilstuna maarufu kama “AFC” ya Sweden ambayo inacheza Ligi Kuu ya nchini humo.

Habari zinasema kwamba uongozi wa Simba umeridhia kiungo huyo mwenye mashuti makali kuondoka na kwenda kusaka maisha nje ya nchi kwa maslahi ya Simba na taifa kwa ujumla.

Mwishoni mwa msimu wa mwaka jana, Simba waligoma Ndemla kwenda kufanya majaribio AFC ya Sweden ambayo anaichezea Thomas Ulimwengu, kwa kuwa walikuwa wakimwitaji.

Samba walitoa sababu kwamba walikuwa wakimwitaji Ndemla katika mechi za mwisho za Ligi Kuu bara pia Kombe la Shirikisho.


Habari zinasema kwamba Ndemla ameshapata visa na anaweza kuondoka wakati wowote kuelekea nchini Sweden ambako haendi kwa majaribio bali kusajiliwa moja kwa moja.

No comments