SALUM MAYANGA AMEAHIDI KUENDELEZA UBABE MBELE YA RWANDA JUMAMOSI HII

KUELEKEA mchezo wa Jumamosi kati ya timu ya Taifa Stars na Rwanda ambao wa kuwania tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la CHAN kwa wachezaji wa ndani, kocha mkuu wa kikosi hicho, Salum Mayanga ameahidi kuendeleza ushindi katika kikosi hicho.

Mayanga amefanya mabadiliko kadhaa katika kikosi hicho baada ya kuwakosa baadhi ya nyota muhimu wanacheza soka nje ya Afrika akiwemo Thomas Ulimwengu, hivyo kumuongeza Kelvin Sabato ambaye ni mara yake ya kwanza kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa.

“Nadhani kila mmoja ameweza kuona jinsi ambavyo kikosi kimeanza kubadilika baada ya kupata uzoefu kwenye michuano ya COSAFA natarajia kuwa tutaibuka na pointi zote tatu,” alisema kocha huyo.


“Unapocheza nyumbani lazima uwe na malengo ya kuibuka na ushindi, naomba Watanzania wajitokeze kwa wingi katika mchezo huo”alimaliza.

No comments