SAMIR NASRI ASEMA "NILIMPUUZA GUARDIOLA ALIPONAMBIA NISIONDOKE MAN CITY"

KUMBE Samir Nasri aliambiwa na kocha wake Pep Guardiola asiondoke lakini straika huyo aliamua kusepa!

Alipoulizwa kwa nini aliamua kuondoka, Nasri alijibu: “Kocha Pep ni mtu kigeugeu na haaminiki, hivyo isingekuwa rahisi kwangu kumkubalia nikabaki maana nisingekuwa na namba ya kudumu.”

“Niliamua hilo kwa maslahi ya kiwango changu cha soka kwa sababu nilikuwa nahitaji kuendelea kucheza kwenye kikosi cha kwanza.”

Kauli hii ya Nasri inakuja wakati huu ambapo anatimiza zaidi ya mwaka unusu hivi ndani ya kikosi cha timu yake ya sasa ya Sevilla inayoshiriki La Liga nchini Hispania.

Katika mazingira yasiyo ya kawaida, Nasri alimeza mate ya akili na kumkatalia kocha wake huyo kwa kile alichodai kuwa uwezekano wa namba katika kikosi cha Manchester City ni mdogo.

Nasri aliingia katika kapu la wachezaji ambao tangu kocha Guardiola atue Manchester City wamekuwa hawana nafasi katika kikosi cha kwanza.

Nasri mwenye umri wa miaka 30, alisema: “Guardiola alitaka nibaki City kwa ahadi ya kuwa nitapata namba kikosini.”
“Lakini nilimkatalia nikitambua kuwa kauli yake haikuwa na ukweli halisi.”

“Mimi ni mchezaji na nahitaji kucheza siku zote ili kulinda kiwango change kisishuke.”


“Nimejiunga na Sevilla katika timu ambayo ni kama familia yangu. Nina uhakika wa kucheza nikiwa hapa.”

No comments