SANCHEZ SASA AJIPELEKA MANCHESTER CITY

NI kama kituko lakini hii si dalili njema kabisa kwa timu ya Arsenal ambayo kama haitachanga vyema karata, inaweza kujikuta inaondokewa na nyota wake katika hatua hizi za mwisho za usajili.

Na mtu ambaye anawatia presha kubwa ni Alexis Sanchez ambaye habari za hivi karibuni zilikuwa zinasema kwamba kocha wake, Arsene Wenger alikataa kumruhusu kuondoka lakini sasa ni kama vile maji yako shingoni kwa mzee huyo wa Kifaransa.

Habari mpya ni kwamba Sanchez sasa anataka kulazimisha kuhamia kwenye klabu ya Manchester City hata kama ni kwa mshahara kiduchu.

Gazeti la The Independent iliandika kwamba, ingawaje kuna habari kuwa nyota huyo anatakiwa sana na Paris Saint-Germain ya Ufaransa lakini kuna uhakika kabisa kwamba njia inaonekana kama ni nyeupe zaidi kwenda Man City.

Imedaiwa kwamba Wenger amekataa kabisa kumruhusu sanches kuondoka na kujiunga PSG lakini kocha huyo hataki kuacha sababu za msingi za kumzuia.

Lakini raia huyo wa Chile amedaiwa sasa kuwa yuko tayari kupokea pesa kiduchu tu ili nadhiri yake ya kujiunga na kocha wake wa zamani Pep Guardiola ambaye walikuwa wote Barcelona na sasa ndie kocha anayeifundisha Man City.

Arsenal wenyewe wamesema kwamba wamekuwa katika hatua nzuri ya kumuongezea mkataba Sanchez lakini straika huyo ametajwa kwamba hayuko tayari kuongeza mkataba.


Juventus na Bayern Munich nazo zimedaiwa kuwa zinaitaka saini ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, ingawaje ni kama bado hajapata nafasi hiyo kwani Man City wanaonekana wako karibu zaidi.

No comments