SASA UNITED IYAAMUA KUFANYA KWELI KWA ALVARO MORATA... yatangaza kumtengea pauni mil 75 kumshawishi

KAMA unadhani Manchester United hawana jeuri ya fedha basi hiyo imekula kwako! Mashetani hao hawataki mzaha hata kidogo kwa mchezaji wanayeona ana thamani ya kuitumikia klabu hiyo.

Katika kuonyesha jeuri ya noti, uongozi wa juu wa United umeweka bayana azma yake ya kutaka saini ya straika Alvaro Morata ambaye kwa sasa anakipiga ndani ya kikosi cha Real Madrid.

Sio kumtaka kwa mali kauli bali wameshaweka bayana kuwa wametenga kitita cha pauni mil 75 kama ushawishi wa mpachika mabao huyo.

Hatua ya winga huyo kuripotiwa kukosa furaha ndani ya Madrid kunaipa nafasi Manchester United ya kufufua matumaini ya kumnasa, ikiwa ni kati ya majaribio yao ya kumnasa.

Ikumbukwe kuwa Morata aliingia kwenye rada za United katika kila kipindi cha usajili, ikiwemo ule wa mwaka 2015 ambapo mashetani hao wekundu walikaribia kumnasa.

Akinukuliwa, bosi wa Manchester United, Jose Mourinho amesema bado anapambana kwa ajili ya kumnasa Morata na kwamba klabu imeshatenga pauni mil 75 za kutua Old Trafford.

“Kila timu kubwa ina malengo ya wachezaji kama Morata, ni winga aliye katika kiwango bora licha ya kutopata nafasi kubwa ndani ya kikosi cha Real Madrid.”

“Tunapambana ili kuhakikisha tunamnasa winga huyu na kumalizana nae katika kipindi kifupi kijacho mara baada ya kufunguliwa kwa usajili wa dirisha hili la kiangazi,” alisisitiza Mourinho.


“Ana nafasi kubwa ya kung’ara akiwa hapa Old Trafford, lakini kikubwa ni kwamba ana uzoefu mkubwa wa soka la England. Hii ndio inayonifanya niamini kuwa ni mchezaji mwenye msaada mkubwa iwapo nitafanikiwa kumshawishi.”

No comments