SENTAHAFU WA JUVENTUS LEONARDO BONUCCI APOKEWA KISHUJAA AC MILAN


Leonardo Bonucci amewasili AC Milan kukamilisha usajili wake wa pauni  milioni 35 akitokea kwa mabingwa wa Serie A, Juventus.

Umati mkubwa wa mashabiki wa Milan ukaibuka kumpokea sentahafu huyo mwenye umri wa miaka 30 huku baadhi yao wakiwa tayari wameshachapisha jina la nyota huyo kwenye jezi zao maarufu zenye mistari ya rangi nyekundu na nyeusi.

Beki huyo aliyeichezea timu ya taifa ya Italia mechi 70, alikuwa akiwaniwa pia na Manchester City na Chelsea.

No comments