SERGIO RAMOS ATUPA DONGO LA "AKILI" KWA JOSE MOURINHO

HILI ni kama dongo kwa kocha mbwatukaji aliyetua katika klabu ya Manchester United, Jose Mourinho.

Safari hii Sergio Ramos alipoulizwa kama ni makocha gani anaowaheshimu, ambao wamewahi kumfundisha, alimweka kando kabisa Mreno huyo.

Ramos ametaja orodha ya makocha bora waliowahi kumfundisha lakini kati yao, jina la Jose Mourinho halimo kabisa na kisha akasisitiza kuwa tangu awe chini ya makocha wa timu alizozitumikia, hajaona ubora wa Mourinho hata kwa kulinganisha na wengine.

Ramos alizungumza hayo baada ya kuulizwa ni makocha wangapi bora waliowahi kumfundisha katika maisha yake ya soka. Jibu likawa: “Carlo Ancelotti ndie kocha bora wa msimu na ndie aliyenifanya niwe katika kiwango cha kujisikia kama nipo nyumbani.”

Ramos mwenye umri wa miaka 28, aliyecheza mara 300 akiwa Madrid, alisema Ancelotti ndie kocha wa mafanikio aliyemwezesha kucheza soka la ufanisi na la kufurahisha.

“Ancelotti ni funguo ya mafanikio na ndio maana ni kati ya makocha wakubwa duniani.”

“Kwa mtazamo wangu ni kati ya makocha wawili bora kwa upande wa maisha yangu ya kisoka, anatambua kukaa na wachezaji na kutambua uwezo wao.”

Alipoulizwa ni kocha gani bora zaidi ya Ancelotti, Ramos alijibu Mourinho bado haingii katika orodha ya makocha bora waliowahi kumfundisha.

“Kuna Luis Aragones kisha yuko Joaquin Caparros ambao waliniamini, wakati huo sikuwa katika kiwango chochote.”  


“Hawa ndio makocha bora kwa upande wangu lakini Ancelotti atabaki kuwa kocha bora wa msimu,” alisisitiza Ramos.

No comments