SEYDON KUACHIA RASMI "SIO POA" WIKI IJAYO

MSANII wa bongofleva, Said Makamba ‘Seydon’ amesema umefika wakati sasa wa kufanya maamuzi ya kuachia audio ya wimbo wake mpya wa ‘Sio Poa’.

Akiongea na Saluti5, Seydon amesema kuwa anatarajia kuiachia audio hiyo mwanzoni kabisa mwa wiki hiyo na kwamba ataisambaza kwenye vituo mbalimbali vya radio.

“Nitaanza kuitambulisha rasmi kwenye radio mbalimbali kabla sijaiachia rasmi,” amesema Seydon na kuwaomba mashabiki waisubirie kwa hamu ujio wake mpya.


“Nitakiachia kibao hicho wakati nikiwa katika harakati za kuandaa kichupa chake ambacho nacho hakitachukua muda mrefu kutoka,” amesema staa huyo

No comments