SHOMARI KAPOMBE ATONESHA MAJERAHA YAKE YA NYONGA

BEKI wa Simba Shomari Kapombe nikama vile anataka kuyeyusha furaha ya mashabiki wa timu hiyo baada ya juzi jumamosi, kutonesha majeraha yake ya nyonga ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.

Kapombe amesajiliwa na Simba hivi karibuni kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Azam FC alikomalizab kandalasi mkatyaba wake.

Beki huyo alitonesha tatizo lake la nyonga baadfa ya ,kuchezewa lafu na Mico Justin wa timu ya taifa ya Lwanda wakati anaitumikia timu yake ya taifa ya Tanzania Taifa Stars mechi iliyochezwa CCM Kirumba na kuwania tiketi ya fainali za ubingwa wa mataifa ya Afrika (Chan).

Akizungumza jana dk wa Taifa Stars, Richard Yombo, alisema kwasasa Kapombe yupo chini ya uangalizi wa madaktari nmkoani Mwanmza kwamuda wa masaa 72 baada ya kumalizika kwa mchezo kabla ya kufanyiwa vipimo kuona kama atawerza kuendelea kuitumikia Stars aun arejeshwe Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.

“Hakuumia kwa maana ya kupata jeraha ra kushona,ila amejitonesha matatizo yake aliyowai kuwa nayo hivyo ndani ya masaa 72 tutakuwa tumejua iwapo ataweza kuendelea kuambatana na timu kwenye mechi ya marudiano au kurejea Dar es Salaam kuangalia jinsi gani atatribiwa.


“Hivi sasa tutaelekea kumpa huduma za hapa na pale kwa muda huu utakao kuwa huku ilikumrejesha kwenye hali yake yakawaida ikitokea tatizo likawa kubwa tunaweza kumsasfilisha kabla ya huo muda” alisema.

No comments