SIKIA HII... MECHI YA MBEAYA CITY NA AZAM FC KIINGILIO JEZI!

KLABU ya Mbeya City imesema itatumia jezi mpya kuwa ni kiingilio uwanjani kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kuchezwa Jumapili hii jijini Mbeya.

Ofisa habari wa Mbeya City, Shaa Mjanja alisema kuwa mchezo huo umeandaliwa kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania bara itakayoanza Agosti 26, mwaka huu.

Alisema, mchezo huo utamsaidia kocha wao, Kinah Phiri kuweza kutambua makosa ya kiufundi kwa wachezaji na kuyasawazisha mapema kabla ya msimu mpya.

Hivyo kwenye mchezo huu wa kirafiki klabu imeona kutumia jezi mpya na bidhaa mbalimbali kama vile skafu kuwa kiingilio uwanjani,” alisema.

Alisema tayari klabu hiyo kupitia wakala maalum imeingiza sokoni jezi na bidhaa muhimu, lengo likiwa ni kuwarahisishia mashabiki na wadau kupata bidhaa hizo.

“Siku hiyo mashabiki na wadau wa soka jijini Mbeya watalazimika kuingia uwanjani kwa tiketi ya jezi au bidhaa yoyote ya klabu ya Mbeya City,” alisema.   Alisema, sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kuitangaza jezi mpya ya timu hiyo na bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa kwa ubora zaidi kupitia kampuni ya Smart Sports.

No comments