SIKILIZA KIBAO “NYUMBA YANGU” CHA SIKINDE, ZAWADI YA MWISHO YA MICHAEL ENOCK KWA SIKINDE


KABLA hajafa, King Michael Enock “Teacher” ambaye alikuwa mwanamuziki mwandamizi wa mlimani Park Sikinde, alidondosha zawadi moja kubwa ambayo ni kibao “Nyumba Yangu” mwaka 1998.

Kama kawaida ya tungo nyingi za Michael Enock, wimbo “Nyumba Yangu” umetengenezwa kwa ufundi wa hali ya juu, hasa kwa upande wa ala ambapo Kassim Rashid “Kizunga” alisimama kwenye gitaa la solo, Huluka Uvuruge (rithym) na Mustapha Ngosha (bass).

Sauti za waimbaji Hussein Jumbe, Nassir Lubua, Shaaban Dede, Tinno Masenge na Abdallah Hemba zimezidi kuupendezesha wimbo huo, wakati drums za Arnold Kang’ombe na tumba za Ally Jamwaka zikionekana kama kachumbari juu ya pilau la biliani.

Kwa bahati mbaya, Michael Enock mwenyewe hakushiriki chochote kwenye “Nyumba Yangu”, lakini alikuwa kiongozi mzuri aliyechangia kuwafanya Shaaban Lendi, Yussuph Benard, Machaku Salum na Milambo kupuliza ala zao za upepo kwa umahiri mkubwa.

No comments