SIKILIZA UTULIVU WA VYOMBO NA SAUTI ZA WAIMBAJI KATIKA KIBAO "CONSOLATA" CHA MLIMANI PARK SIKINDE

UELEWANO mzuri wa magitaa ya Ramadhani Mapesa, Fadhili Uvuruge na marehemu Mustapha Ngosha umechangia kwa kiasi kikubwa kuleta ladha ya aina yake kwenye ala za wimbo “Cosolata” wa Mlimani Park Sikinde uliorekodiwa mwaka 1998.

Wimbo huu ni utunzi wa marehemu Adam Bakari “Sauti ya Zege” na unapatikana kwenye albamu ya “Nyumba Yangu” inayokusanya pia vibao “Mtoto Sarah”, “Chozi la Kejeli” na “Femia” ambacho pia ni makucha ya Sauti ya Zege.

Waimbaji kwenye wimbo huu ni Hussein Jumbe, Nassir Lubua, Abdallah Hemba na Adam Bakari mwenyewe ambaye uzito wa sauti yake unaleta raha isiyo kifani kwenye kazi hiyo ambayo drums zake zimecharazwa na Arnold Kang’ombe na tumba Ally Jamwaka.

No comments