SIMBA YACHOMOA KUSAJILI WACHEZAJI WAWILI "MAMLUKI" WA YANGA

WAKATI ambapo klabu ya soka ya Simba ikiendelea na zoezi la usajili, kuna taarifa kuwa wachezaji wawili kutoka ndani ya kikosi cha Yanga wamekwama kupata nafasi ya usajili ndani ya kikosi cha "Mnyama".

Chanzo makini cha habari za usajili wa msimu kimeiambia saluti5 kuwa wachezaji hao waliomba kusajiliwa Simba lakini kamati ya usajili iliyo chini ya kamanda Zacharia Hans Poppe imewatolea nje.

Hata hivyo taarifa hizi zimeminya majina ya wachezaji kuanikwa mtandaoni kwa sababu maalum.

Imebainika kuwa awali majina ya wachezaji hao yalikuwa yanatajwa kwa orodha ya wanadhinga wapya waliokuwa na nafasi kubwa kusajiliwa katika kikosi cha msimu ujao cha wekundu wa Msimbazi lakini wamekataliwa kutokana na kuhofia kuwa mamluki.

Kukwama kwa wachezaji hao  kunatokana na kinachotajwa kuwa kamati ya usajili ya Wanamsimbazi imekuwa makini katika kufiatilia vigezo mbambali vya wachezaji wapya ikiwemo suala la uaminifu wa dhati la kuitumikia timu kwa moyo.

“Kamati imekuwa makini sana katika zoezi la usajili linaloendelea, kubwa ni kujiaminisha kama wanaosajiliwa wana moyo wa dhati wa kuitumikia Simba.”


“Vigezo hivi ndivyo vinavyofanya usajili wa msimu huu kuwa makini na hii inatokana na ukweli kuwa baadhi ya wachezaji wa msimu ulliopita walishindwa kuitumikia timu kwa mapenzi hivyo walichangia kuifanya Simba kukosa ubingwa na uwakilishi wa michuano ya kimataifa mwakani,” kilisema chanzo makini cha habari hizi.

No comments