SIMBA YAFANIKIWA KUWASHAWISHI ABDI BANDA, JUUKO MURSHID KUBAKI MSIMBAZI

IMEBAINIKA kuwa mabeki wawili wagumu katika kikosi cha Simba Abdi Banda na Juuko Murshid hawaondoki katika kikosi cha Simba.

Awali kulikuwa na wasiwasi kwamba Banda anakwenda kucheza soka nchini Afrika Kusini na Juuko ambaye ni beki wa timu ya taifa ya Uganda anakwenda nchini Serbia.

Lakini sasa wapenzi wa Simba wametakiwa kutokuwa na wasiwasi baada ya kiongozi mmoja kutamka kwamba mabeki hao wa kati wanaobaki Simba.

Kiongozi huyo amesema kwamba mabeki hao wamefikia makubaliano na uongozi na kuwahakikishia kwamba hawataondoka.

“Banda ilikuwa asajiliwe na klabu ya Polokwane ya Afrika Kusini lakini sasa kuna uhakika kuwa anabaki Simba, Juuko nae pia ameshauriwa abaki Simba kwa msimu mwingine,” kimesema chanzo hicho.

Hata hivyo, kiwango cha Banda anachoonyesha kwenye michuano ya Kombe la mataifa ya kusini mwa Afrika (COSAFA), inayofavyika nchini Afrika Kusini, kimewavutia mawakala wengi.


Mwishoni mwa wiki iliyopita kulikuwa na taarifa kwamba Simba iko katika hatari ya kuwapoteza wachezaji wake watatu wa kutumainiwa ambao ni Banda, Kichuya na Yasin ambao wamekuwa wakiwindwa na baadhi ya timu za Afrika Kusini.

No comments