SIMBA YAMNYATIA KIUNGO ALLAN KATAREGGA WA AFC LEOPARDS

SIMBA iko katika mipango madhubuti ya kusajili na kuunganisha kikosi chake upya.

Na kama ambavyo siku zote wanafanya, wekundu hao wa Msimbazi wameonekana kufanya usajili wao kwa umakini wa hali ya juu.

Moja ya mawindo ambayo Simba inanyatia kwa sasa ni kumnasa kiungo Allan Katerega wa AFC Leopards ya Kenya, ambaye aling’ara sana katika michuano ya Sportpesa Super Cup jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa viongozi wa Simba ameithibitishia saluti5 kwamba Katerega anaweza kuwa mmoja wa wachezaji wapya wa Simba kama mipango iliyosukwa itakwenda kama ilivyopangwa.

Amesema kwamba Simba inamtaka kiungo huyo kwa ajili ya nafasi ya ushambuliaji kama mipango ya kumsajili Walter Bwalya itakuwa haijakaa sawa.


Bwalya ambaye amekiri kwamba amefikia mahali pazuri na Simba ingawa anawekewa ngumu na baadhi ya viongozi wa soka nchini Zambia wakisema kwamba sio raia wa nchini hiyo.

No comments