"SIO RAHISI TENA KWA ARSENAL KUENDELEA NA SANCHEZ"

BAADHI ya magazeti makubwa nchini Uingereza yanasema kwamba hata kama watatumia mitutu, lakini sio rahisi kwa Arsenal kuendelea kuwa na nyota wake Alexis Sanchez.

Ijumaa iliyopita  mshambuliaji huyo nyota raia wa Chille aliandika katika ukurasa wake wa Instagram akisema kwamba anaumwa na ameshauriwa kuwa apunzike.

Alikuwa amepiga picha akiwa na mbwa wake wakiwa wamepuinzika kwenye sofa na kusema kwamba anaumwa.

Mtandao mmoja umeandika kwamba hakuna haja ya kuhoji kama kweli Sanchez anaumwa ama la lakini wapenzi wa Arsenal wamejawa na wasiwasi hasa ikizingatiwa kwamba hakuwa na msimu mzuri katika kikosi hicho akitaka kuondoka.

Nyota huyo wa zamani wa Barcelona alikuwa akisubiriwa kujiunga na kikosi cha wachezaji wenzake katika kambi ya mazoezi ngumu kwake kujiunga na wenzake kwa sababu anaumwa.

Hata hivyo, mchezaji huyo anahusishwa kuondoka katika timu hiyo na kuhamia katika klabu za ama Manchester City au Paris Saint Germain ambazo zimekuwa katika nafasi kubwa za kumsajili.


Mtandao wa Off The Post umeandika kwamba sanchez anaweza kuwa hana tatizo lolote lakini tabia yake ya msimu mzima uliopita inamuondoa kwenye kuaminiwa.

No comments