SOLANKE ALIYETOKEA CHELSEA AAHIDI MAKUBWA LIVERPOOL


LIVERPOOL imetangaza kumsainisha kinda Dominic Solanke baada ya mkataba wake kufikia ukomo Chelsea na atavaa jezi namba 29, huku akisema kuwa ana kiu ya kuandika historia katika klabu hiyo.


Nyota huyo wa miaka 19 anayecheza kama straika, huku akimudu pia nafasi ya winga na kiungo mshambuliaji, ameuambia mtandao wa klabu hiyo kuwa amefurahia kujiunga na Liverpool na kila mmoja amemfanya kuhisi kuwa tayari amekaribishwa Anfield.

No comments