STAA WA KIKE WA NOLLYWOOD AIBUKA NA KUDAI WANAUME WA KINAIGERIA SI WAAMINIFU KWENYE MAPENZI

STAA wa filamu nchini Nigeria, Sylivia Edem amewageukia wanaume wa taifa hilo na kudai kuwa hawana uaminifu katika suala zima la mahusiano ya kimapenzi.

Edem amesema kwamba ameshaingia kwenye uhusiano wa kindoa na wanaume wawili lakini mwisho wa siku aliambulia maumivu kutoka kwao.

“Niweke wazi tu kuwa labda itokee nimepata mwanaume wa kizungu, naweza kuishi nae, lakini hawa ndugu zangu wa hapa sina tena imani nao hata kidogo, alisema staa huyo.

“Nimeishi na wanaume wawili na wote walikuwa na matatizo yanayofanana na hivyo ni bora nibaki kama nilivyo, sina imani na wanaume wa nchi hii.”


“Nimejaribu kwenda wanavyotaka wao lakini nimeshindwa, nilikuwa naumia kila leo. Nimechoka na nitaishi peke yangu labda atokee mtu wa rangi tofauti,” alimaliza.                                                                                                                                                                                                                                                                                   

No comments