STAA WA MUVI GHANA AANIKA PICHA ZA MAPACHA ALIOWAZAA NA BABA MTOTO WAKE

MCHEZA filamu mwenye mvuto nchini Ghana, Nadia Buari ameanza kuanika picha za watoto wake mapacha sambamba na baba watoto wake kwenye mtandao wa kijamii.

Buari alikuwa akificha picha hizo kwa kisingizio cha kutotaka mambo yake binafsi yafahamike na jamii.

Staa huyo alijifungua watoto hao mapacha mwaka 2015 akiwa nchini Marekani na tangu wakati huo hajawahi kuonekana nao hadharani.


Lakini hivi sasa inaonekana ameanza kuachana na msimamo huo baada ya kuweka picha mtandaoni akiwa anaongozana na mzazi mwenzie na watoto wao hao.

No comments