TAMBWE: UJIO WA AJIB YANGA HAUNIPI HOMA YA KUKOSA NAMBA KIKOSI CHA KWANZA

MSHAMBULIAJI wa mabingwa wa Yanga, Amissi Tambwe amesema hana mashaka katika namba katika kikosi cha kwanza kwa timu hiyo baada ya kusajiliwa Ibrahim Ajib aliyejiunga akitokea Simba.

Nyota huyo mwenye rekodi nzuri ya ufungaji katika kikosi hicho alisema anafurahi zaidi ujio wa Ajib kuliko watu wanavyofikiria.

“Suala la nani atacheza kwenye kikosi cha kwanza lipo mikononi mwa kocha mkuu hivyo siwezi kuumiza kichwa juu ya hilo, mimi kama mchezaji nimejipanga kuhakikisha naisaidia klabu yangu kufanya vyema msimu ujao,” alisema Tambwe.

“Ujio wake ni mzuri nimejipanga kushirikiana nae katika mechi zote.


No comments