THIAGO ALCANTARA ASEMA HAKUNA TOFAUTI KATI YA BEYERN MUNICH NA REAL MADRID


REAL MADRID ni klabu bora barani Ulaya, ikiwa na wachezaji wenye majina makubwa kama ilivyo kwa Barcelona, huku ikishinda mataji kibao barani humo, lakini Thiago Alcantara amesema haoni tofauti yoyote kati ya klabu hizo na Bayern Munich katika suala la ubora.

"Ukilinganisha timu, pia tuna mastaa wa kiwango cha dunia,” alisema Alcantara alipoulizwa na gazeti la Bild kwamba anailinganisha vipi Bayern na klabu mbili zinazotajwa kuwa bora zaidi barani Ulaya - Madrid na Barcelona.

Alcantara aliyejiunga na Bayern Munich mwaka 2013 akitokea Barcelona, alisema timu hizo zimekuwa zikitumia fedha nyingi kusajili, lakini wao wamechagua kununua makinda yenye vipaji.

 "Hakuna tofauti katika ubora. Tupo katika daraja sawa, asilimia 100... Lakini jambo moja ni uhakika, katika chumba cha kubadilishia nguo hatuzungumzi kuhusu mastaa wa dunia isipokuwa kuhusu ari ya timu.

"Si muhimu kutumia fedha nyingi. Kuna wachezaji kibao wenye vipaji vikubwa ambao bado wanahitaji kufuatiliwa. Hiyo ndiyo njia ya Bayern Munich – kusaini mchezaji na kumjenga,” alisema.

No comments