THIBAUT COURTOIS ATIKISA KIBIRITI CHELSEA... ataka mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki

THIBAUT Courtois ameanza kuitikisa klabu ya Chelsea akitaka mshahara wa pauni 200,000 kwa wiki ili aingie kwenye daraja la wachezaji wanaolipwa mkwanja mrefu Stanford Bridge.

Inakuwa kama hadithi lakini huo ndio ukweli wenyewe, anataka kufanana na wachezaji wenye hadhi kubwa kama Eden Hazard, Wayne Rooney, au Yaya Toure ambao wapo kwenye madaraja hayo kwa mishahara.

Roman Abrahamovich anamlipa pauni 90,000 kwa wiki lakini yeye anaona ni fedheha kupokea fedha hiyo, anaamini ameshakomaa na anastahili kulingana na nyota wakubwa ambapo anahitaji kulipwa mara mbili ya mshahara anaopata sasa ili aendelee kubaki Stanford Bridge.

Anafahamu namna ambavyo Real Madrid wanamtamani hivyo anatumia ndoano hiyo kuitikisa Chelsea.

Ni jambo la kushitua kidogo, hasa kwa wachezaji wanaocheza nafasi ya mlinda mlango, si jambo lililozoeleka sana. 

Imezoeleka kuona washambuliaji na mawinga ndio hulipwa fedha nyingi lakini sio kwa mabeki, makipa na viungo wakabaji kama N’Golo Kante.

Mwaka jana kipa David de Gea alitikisa kiberiti akataka kutua Real Madrid, Manchester United ikampa mkataba mpya na kumlipa kiasi cha pauni laki mbili kwa wiki.

Ilikuwa ni habari kubwa kwa sababu makipa hata wawe na ubora wa kiasi gani bado huhesabika kama wachezaji wasiokuwa na umuhimu sana.

Unapoona makipa nao wameamka na kutaja madau makubwa ujue tunakoelekea ni kubaya sana, kila nafasi uwanjani itahitaji kulipwa kitita kikubwa cha fedha na matokeo yake soka litabaki mikononi mwa matajiri wachache wenye uwezo wa kulisimamia.


Kinda kama Thibaut anataka kulipwa fedha nyingi kumzidi Buffon wa Juventus ambaye amebeba makombe mengi na mwenye uzoefu mkubwa, ni jambo la kusikitisha kidogo.

No comments