THIERRY HENRY ASEMA LIONEL MESSI BADO YUKO GADO

NYOTA wa zamani wa  Barcelona na timu ya Taifa ya Ufaransa,  Thierry Henry amesema kuwa staa mwenzake,  Lionel Messi bado ana uwezo wa kuimarika zaidi na kukabiliana na msimu ujao.

Kwa sasa kikosi hicho cha Ernesto Valverde, bado kinaendelea vizuri na ziara yake  mjini  New York, ya kujiandaa na msimu ujao, baada ya mwishoni mwa wiki kuondoka na ushindi wa mabao  2-1 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Juventus.

Huku wengine wakiwa wameshikwa na kihoro kuhusu msimu ujao, Henry anampongeza Muargentina huyo kwa ndoto zake za kutaka kucheza na kufanya mazoezi kila siku kwa bidii.

Mbali na kumpongeza staa huyo  wa zamani ambaye kwa sasa ni Balozi wa klabu hiyo ya  Catalan alisema kwamba ulimwengu wa soka bado haujamalizika kushuhudia Messi akiendelea kuwa bora.

"Kwa sasa anatengeneza mabao mengi na ninadhani watu hawazungumzi mambo mengi ambayo anayafanya kwa ajili ya timu,”  Henry alikiambia kituo cha  Barca TV.


"Messi amekuwa akiimarika zaidi na zaidi na  ni mchezaji mwenye maajabu makubwa,”aliongeza staa huyo wa zamani.

No comments