TOTTENHAM, LIVERPOOL ZAINGIA VITANI KUWANIA SAINI YA KIUNGO WA DORTMUND

KIUNGO Mahmoud Dahoud ameziingiza vitani klabu za Tottenham Hotspurs na Liverpool ambazo kila moja inasaka saini yake kiangazi hiki.

Dahoud mwenye uraia wa Syria amekuwa muhimili wa idara ya ushambuliaji na tayari Spurs wamekuwa wa kwanza kuingia katika mbio za kumsajili tangu lilipofunguliwa dirisha la majira ya joto.

Pamoja na Spurs na Liverpool, Dahoud amewavuta mabingwa watetezi wa serie A, Juventus ambao nao walianza kufanya mazungumzo nae tangu katika usajili wa majira ya baridi, lakini dili hilo halikukamilika.

Dahoud alizaliwa nchini Syria jirani na mpaka wa Uturuki na amekulia katika kituo cha kukuzia vipaji klabu ya Gladbach akitokea katika timu ya Fortuna Dusseldorf mnamo mwaka 2010.

Hata hivyo, taarifa kutoka ndani ya klabu yake ya sasa zinathibitisha kuwa kiungo huyo ana mkataba wa muda mrefu unaofikia tamati mwaka 2018, ingawa tayari wameanza mazungumzo ya awali ya kumuongezea kandarasi mpya.

Magazeti ya nchini Ujerumani yamethibitisha taarifa kuwa, Spurs wameshaanza mazungumzo na klabu ya Dortmund.


No comments