TOTTENHAM YAKANA KUWA KWENYE MAZUNGUMZO YA KUMUUZIA TIMU MMILIKI WA MTANDAO WA FACEBOOK

UONGOZI wa Tottenham umekanusha kuwa wako kwenye mazungumzo na mmiliki wa mtandao wa kijamii wa Facebook, Mark Zuckerberg juu ya kumuuzia klabu hiyo.

Awali kulikuwa na taarifa kuwa Mark amewafuata kwa nia ya kuinunua Spurs na amewaahidi pauni mil 1.

Ilielezwa kuwa kampuni ya Iconiq Capital ya Marekani inayofanya kazi na tajiri huyo ndiyo iliyopanga kutoa kitita hicho.

“Bodi haipo kwenye mazungumzo yoyote yanayohusiana na kuuzwa kwa klabu,” ilisema taarifa ya klabu hiyo yenye masikani yake Kaskazini mwa jiji la London.


No comments