"TUTABANANA HAPAHAPA REAL MADRID" GARETH BALE ASEMA

UNAWEZA kusema ni kama katangaza vita baada ya straika Gareth Bale kusema kuwa hajawahi kufikiria kuitema Real Madrid na huku staa huyo raia wa Wales akisema kuwa yuko tayari kupigania namba yake katika kikosi hicho cha mabingwa wa Hispania na Ulaya.

Kauli ya staa huyo imekuja wakati akiendelea kuhusishwa kuitema Real Madrid na huku vinara wa soka England, Manchester United wakiripotiwa kumwania.

Kwa sasa hatma ya nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 inaonekana kuwa shakani kutokana na kuwa Real Madrid bado wanaendelea kumshawishi staa wa Monaco, Kylian Mbappe lakini Bale anasema kuwa hata akija hana mpango wa kuondoka kwa mabingwa hao wa La Liga na Ligi ya mabingwa Ulaya.

“Sina mawazo ya kuondoka Real Madrid,” Bale aliliambia gazeti la Marca. “Kwa ukweli sisomi tetesi hizo.”

“Kwa ujumla mimi ni mchezaji raia wa Uingereza na mara zote nimekuwa nikihusishwa kurejea nyumbani. Imewahi kutokea kwa David Beckham na wachezaji wengine wa Uingereza ambao wamewahi kuja Hispania, hivyo hakuna jipya,” aliongeza staa huyo.


Alisema kwamba anajisikia mwenye furaha kucheza soka nchini Madrid na kwamba kwa sasa hakuna ofa inayomwitaji.

No comments