UJERUMANI YAKOMAA NA NA KOCHA WAO JOACHIM LOEW MPAKA KIELEWEKE

SHIRIKISHO la kandanda Ujerumani (DFB), limeweka baya azma yake ya kuendelea na kocha wa timu ya taifa wa nchi hiyo, Joachim Loew.

Hatua hiyo imefuatia taarifa kuwa kocha huyo yu njiani kuachana na timu ya taifa baada ya kuipa ubingwa wa mabara katika michuano iliyomalizika hvi karibuni ichini Urusi.

Lakini DFB wamekanusha vikali uvumi huo na kusisitiza kuwa wataendelea kuwa na mwalimu huyo hasa katika kipindi hiki cha kujiandaa na mashindano ya fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018.

Rais wa DFB, Reinhard Grindel ndiye aliyethibitisha haya akivitaarifu vyombo vya habari vya nchini Ujerumani.


“Kwa heshima ya kocha wetu bingwa wa dunia, Jogi 
anapaswa kuamua binafsi. Iwapo anataka kufanya uamuzi mara tu baada ya fainali za Kombe la Dunia nitasema tufanye hivyo,” alisema Grindel.

No comments