UNAAMINI KUWA NYOSHI ALIKUWA NA MIPANGO YA KUITOSA FM? SIKILIZA HII AUDIO


Baada ya Nyoshi el Saadat kuenguliwa urais wa bendi ya FM Academia, nafasi yake ikichukuliwa na Patcho Mwamba, kuna mengi yanazungumzwa ikiwemo shutma kuwa Nyoshi alikuwa anajipanga kuanzisha bendi yake.

Shutma hizo zikashereheshwa na maneno ya kimjini kuwa Nyoshi katumbuliwa kabla hajaibomoa FM …kawahiwa!

Siku moja kabla Nyoshi hajaenguliwa kwenye nafasi hiyo, alitembelea Saluti5 na kufanya mahojiano marefu kwaajili ya kupromoti kazi mpya zijazo za FM Academia.

Tunaweza kujinadi kuwa haya yalikuwa mahojiano ya mwisho kwa Nyoshi el Saadat na chombo chochote kile akiwa rais wa FM Academia.

Sikiliza audio ya sehemu ya maongezi ya Nyoshi na Saluti5 halafu utapata picha iwapo ni kweli alikuwa mipango ya kuitosa FM Academia au la.

No comments