MANCHESTER UNITED itakataa ofa mpya ya pauni milioni 60 kutoka kwa Real Madrid inayotaka saini ya kipa David de Gea.

Mabosi wa Real Madrid wanatarajiwa kuibuka na ofa ya pauni milioni 60 kwaajili ya mlinda mlango huyo wa kimataifa wa Hispania, hatua inayotegemewa kuzidi kuchafua hali ya hewa baina ya vilabu hivyo viwili.

Manchester United haikufurahishwa na namna Real Madrid walivyotia ngumu usajili wa mshambuliaji Alvaro Morata aliyekuwa akiwaniwa kwa udi na uvumba na United.

Manchester United na Real Madrid zote ziko  Los Angeles, Marekani kwenye ziara ya maadalizi ya msimu mpya na kwa pamoja zimeweka kambi kwenye uwanja wa mazoezi wa UCLA.

United imeweka wazi kuwa De Gea hauzwi lakini Real Madrid wanajipa moyo kutokana na utashi wa kipa huyo kutamani kurejea katika jiji la Madrid.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac