USAIN BOLT ASEMA MANCHESTER UNITED ITAJIPINDA KUHAKIKISHA ZLATAN ANABAKI KIKOSINI MSIMU UJAO

MKIMBIZA upepo mahiri duniani ambaye ni shabiki mkubwa wa  Manchester United, Usain Bolt, amesema kwamba klabu hiyo ya Old Trafford itahakikisha inafanya kila liwezekanalo ili straika wao Zlatan Ibrahimovic msimu ujao awepo kwenye kikosi hicho.

Staa huyo ambaye amewahi kunyakua medali kadhaa za michuano ya Olimpiki, alisema juzi kwamba anasema hivyo kutokana na anavyoamini Ibrahimovic ni kati ya mastraika bora duniani.

“Wanatakiwa kumsainisha tena  Ibrahimovic ni moja kati ya mastraika bora," alisema Bolt baada ya kutwaa medali ya dhahabu katika michuano ya Ligi ya Diamond inayofanyika katika mji wa Monaco, nchini Ufaransa.

"Kwangu mimi msimu uliopita alikuwa vizuri na endapo kama ningeambiwa nimpe tena nafasi, ningemsajili,” aliongeza mkimbiza upepo huyo.


Hadi sasa Ibrahimovic hana klabu baada ya kupata majeraha makubwa ya goti mwishoni mwa msimu uliopita wakati akiitumikia Man United.

No comments