USAJILI WA ANTONIO RUDIGER CHELSEA WAMPA JEURI CONTE


ANTONIO RUDIGER aliyekamilisha uhamisho wa pauni milioni 34 kujiunga na Chelsea kwa mkataba wa miaka mitano akitokea AS Roma, amempa jeuri kocha Antonio Conte.

Sasa beki huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 24, anakuwa nyota wa pili kusajiliwa Chelsea kiangazi hiki baada ya kipa wa Manchester City, Willy Caballero.


Conte amesema kwa usajili wa Rudiger,  amemaliza kazi ya kujenga ukuta wake na sasa anaelekea katika upande wa kiungo na ushambuliaji.

No comments