USAJILI WA THOMAS LEMAR ARSENAL WAFIKIA PATAMU, MONACO WATOA TAMKO


Kama ulidhani Arsenal itamsajili kirahisi Thomas Lemar wa Monaco basi andika maumivu.

Monaco imesema Lemar hatauzwa kiangazi hiki licha ya Arsenal kutenga pauni milioni 50 ili kumnasa winga huyo.

Makamu mwenyekiti wa Monaco, Vadim Vasilyev amesema kwenye mkutano wa waandishi wa habari kuwa  Lemar hauzwi na hata kiungo Fabinho naye pia hayuko sokoni.

No comments