UWEZO WA MCAMEROON FENANDO BONGNYANG WAMKWANGUA ROHO KOCHA GEORGE LWANDAMINA YANGA SC

KOCHA wa Yanga, George Lwandamina amekamilisha mazoezi ya gym kwa wachezaji wa kikosi chake waliopo hivi sasa, lakini amegundua jambo moja zito kwamba kati ya wageni wapya waliotua Jangwani, yumo Mcameroon Fenando Bongnyang ambaye ni noma sana.

Staa huyo aliyekuwa akiichezea Cotton Sports alitua hivi karibuni akiwa mchezaji huru kwa maelezo kwamba mkataba wake umemalizika na ameletwa na mmoja wa mawakala wa Yanga ingawa kuna taarifa kuwa kocha ndie atakayetoa maamuzi ya mwisho.

Faili la mchezaji huyo linaonyesha kuwa amekulia kwenye “akademi” mbalimbali na sifa yake kubwa kwa mujibu wa gazeti la Cameroon ni mpaka rangi kwenye kiungo na mchezaji mwenye sifa ya kuchezesha timu na kupiga pasi za kupenyeza.

Staa huyo inaelezwa kuwa ana uwezo mkubwa wa kukaba na sasa amevuruga kabisa mipango ya Lwandamina aliyekuwa na majina mawili kwenye faili lake ambayo ni Kabamba Tshishimbi aliyekuwa akimuangalia nchini Swaziland Jumapili iliyopita na Cletius Chota Chama wa Zambia.

Habari zinasema kwamba viongozi wa yanga wameangalia uwezo wa mchezaji huyo kupitia video na rekodi zake wakafurahi, ingawa hawana mamlaka yoyote juu ya Lwandamina.

Rekodi za mchezaji huyo ambae Yanga wanamfanya siri kubwa zinaonyesha kuwa amekuwa tegemeo kubwa kwa timu ya taifa ya Cameroon ya wachezaji wa ndani na aliwahi kupata dili kadhaa akatoka nje lakini akarudi.

Yanga wamekuwa wakifanya ujio huo siri kwa kuhofia kufanyiwa fojo na watani zao kutokana na kiburi cha fedha cha mfadili wao, mohammed Dewji “MO”.

Kwa mujibu wa mmojo wa viongozi wa Yanga mwenye ushawishi kwenye kamati ya usajili, ni kuwa ujio wake kama ukikubaliwa na kocha utafuta nyayo za Haruna Niyonzima ambaye ameibukia Simba licha ya kwamba hawajamtangaza.


Pia inaharakisha Yanga kuachana rasmi na mkata umeme ambaye alishindwa kuonyesha makeke katika kipindi chote alichokuwa.

No comments