VANESSA MDEE ACHEKELEA KOLABO NA PETER OKOYE WA P-SQUARE

MODO wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, Vanessa Mdee ameonyesha furaha yake baada ya kupata fursa ya kufanya kolabo na staa wa Nigeria, Peter Okoye ambaye ni memba wa kundi la “P-Square”.

Vanessa amefanikiwa kufanya ngoma ya “Kisela” na staa huyo aliyefanikiwa kimuziki na kuteka soko la dunia.

“Kwa kusema kweli hakuna jitihada zozote ambazo nimefanya ili kumpata Peter Okoye, ilitokea tu ghafla tumekutana hotelini nikiwa bize na masuala yangu ya kimuziki akaomba kuongeza mashairi yake kwenye wimbo wangu mpya,” alisema Vanessa.

“Imekuwa ni bahati kwa sababu sikutarajia kwa mazingira tulivyokutana nae angeweza kushawishika kufanya kazi ya muziki na mimi,” aliongeza staa huyo.


Vanessa ndie staa wa kike anaetajwa kufanya vizuri zaidi kwenye muziki wa kizazi kipya baada ya Lady Jaydee huku pia kapo yake na Jux ikionekana kuwa imara zaidi.

No comments