VANESSA MDEE AWAWEKA MKAO WA KULA MASHABIKI WAKE... asema muda si mrefu "ataliamsha dude" kwa kutoa kazi mpya

UMEMISS kusikia ngoma mpya kutoka kwa Vanessa Mdee? Basi kaa mkao wa kula.

Ni takriban miezi sita tangu mrembo huyo wa bongofleva alipoachia wimbo wake wa “Cash Madame”, kipindi chote hicho ameonekana kuwa kimya kwenye kuachia nyimbo zake na badala yake ameonekana akishirikishwa kwenye kazi nyingi mfululizo zilizotoka hivi karibuni.

Vanessa kupitia mtandao wa Instagram amewashitua mashabiki wake kwa kuwaweka tayari kuwa muda si mrefu anakuja kuliamsha dude kwa kuachia ngoma yake mpya.


Mwimbaji huyo ameshafanya kazi kadhaa ambazo ziko tayari, ikiwemo aliyoshuti video na Navio wa Uganda mwezi uliopita.

No comments