VARDY ASEMA HAJUTII KUPOTEZEA OFA YA ARSENAL NA KUAMUA KUBAKI LEICESTER

STRAIKA Jamie Vardy ni kama amezidi kuipotezea Arsenal baada ya kusema kuwa hana cha kujutia juu ya uamuazi wake wa kubaki na mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu England, Leicester City.

Kwa sasa zimebaki takribani siku 49, kabla ya Vardy  kuwaongoza mbwa mwitu  hao katika mechi yao ya kwanza dhidi ya  Arsenal ikiwa ni baada ya Gunners kujaribu kumsajili wakati wa ligi ya msimu uliopita kumalizika.

"Sina chochote cha kujutia, kwani nilifanya uamuzi mzuri katika maisha yangu,” Vardy aliyaambia magazeti ya Uingereza.

"Tangu niwe mahali hapa tumekuwa tukicheza kwa maringo ya kutwaa ubingwa, kupambana tusishuke daraja na ili kujizuia kushuka daraja ni lazima upiganie kuwa katikati mwa msimamo wa ligi,” aliongeza staa huyo.


Alihoji kwa sasa nani anaweza kufahamu kama wanaweza kuwa na msimu mwingine mzuri? Na huku akisema kuwa ngoja wasubiri ili waone na kwamba mipango ya klabu yao wanawataka kumaliza wakiwa katika nafasi hizo na hivyo wamejipanga kuhakikisha wanafanya kila liwezekanalo ili kumaliza wakiwa eneo hilo.

No comments