WAGANDA KUCHEZESHA MECHI YA STARS NA RWANDA LEO

SHIRIKISHO la mpira wa miguu Afrika (CAF), limewateua waamuzi wa Uganda kuchezesha mchezo wa marudiano kati ya timu ya taifa ya Rwanda “Amavubi” na Taifa Stars ya Tanzania kuwania tiketi ya kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ligi za ndani (CHAN).

Stars na Rwanda zinarudiana leo Jumamosi kwenye uwanja wa Nyamilambo mjini Kigali baada ya kutoka sare ya bao 1-1 jijini Mwanza wiki iliyopita na timu inayoshinda ndio itakayofanikiwa kusonga mbele.

Mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua utachezwa saa 10:00 jioni kwa saa za Rwanda ambazo ni sawa na 9:00 alasiri kwa saa za Tanzania na utachezeshwa na Brian Nsubuga Miilo ambaye ni raia wa Uganda atakayepuliza kipyenga cha kati.

Atasaidiana na Ronald Katenya (Line 1), pamoja na Dick Okello (Line 2), wakati mwamuzi wa akiba atakuwa Cheleneti Ally Sabila hukukamishina wa mchezo atakuwa ni Ally Ahmed Mohammed kutoka Somalia.


Stars ina matumaini ya kusonga mbele kutokana na rekodi yake ambapo hadi sasa imecheza jumla ya mechi 10 za kimataifa, imeshinda mechi nne, sare tano na kupoteza mchezo mmoja wa nusu fainali ya michuano ya COSAFA.

No comments