WAYNE ROONEY AMUONYA LUKAKU MANCHESTER UNITED


Wayne Rooney amesema uimara wa akili ndiyo kipimo kikuu kwa  Romelu Lukaku ndani ya Manchester United na kuonya kuwa mambo yamekuwa magumu kwa wachezaji wapya wanaosajiliwa  Old Trafford  miaka ya sasa kulinganisha na mwaka 2004 aliojiunga na Mashetani hao wekundu akitokea Everton.

Rooney ambaye wiki iliyopita alirejea Everton huku Lukaku akienda Manchester United, amemtahadharisha mshambuliaji huyo wa Kibelgiji mwenye miaka 24 kuwa kila udhaifu utakaojitokeza kwake basi lazima utaanikwa ndani ya klabu hiyo kubwa England.

"Kuichezea Manchester United ni changamoto ya hadhi," alisema Rooney. Unapaswa kuwa imara kiakili na kukubali kukosolewa. United ni klabu inayotaka mafanikio. Romelu anapaswa kuwa imara kiasi cha kutosha ili kuzishinda changamoto.

"Kama atakuwa imara kukabiliana na changamoto basi atafanikiwa sana. Akihofia vitu kama hivyo  mambo yatakuwa magumu."

Rooney alikuwa na miaka 18 wakati alipojiunga na United lakini akafanikiwa kuzoa mafanikio makuwa ikiwemo ya kuibuka kuwa mfungaji anayeongoza kwa magoli mengi katika historia ya klabu hiyo sambamba na kutwaa mataji ya Ulaya na England.
No comments