WAYNE ROONEY APELEKWA BURE EVERTON


Manchester United yampeleka Wayne Rooney bure Everton 
ambapo wakala wa nahodha huyo, Paul Stretford, Jumatano mchana alionekana nje ya ofisi za mmiliki wa Everton Bill Kenwright.

Inaaminika Paul Stretford alikuwepo hapo kukamilisha mazungumzo ya usajili wa Rooney huku sharti pekee kwa Everton ni kuendelea kulipa mshahara wa pauni 230,000 aliokuwa akilipwa Rooney Old Trafford.

Uhamisho wa Rooney kurejea Everton ndio unaoaminika kuwa umelainisha safari ya Romelu Lukaku kuelekea Manchester United kwa pauni milioni 75.

No comments