WAYNE ROONEY ATAKA EVERTON ICHUKUE VIKOMBE... asema "tunachukua hatua kubwa kuhakikisha kuwa tunashinda vikombe"

STRAIKA Wayne Rooney anasema kuwa kushinda Kombe na Everton kitakuwa kilele cha ufanisi baada ya kujiunga na klabu hiyo akitokea Manchaster United.

Rooney anaitaka Everton kushinda Kombe lao kuu la kwanza tangu ishinde mwaka 1995 Kombe la FA.

“Klabu hii inastahili kushinda vikombe na tunachukua hatua kubwa kuhakikisha kuwa tunashinda vikombe,” alisema Rooney.

Everton imetumia pauni mil 90 msimu huu katika kununua ardhi huko Liverpool ambapo watajenga uwanja kwa gharama ya pauni mil 300.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anavaa jezi namba 10 ambayo ilikuwa ya Romelu Lukaku ambaye alijiunga na Manchester United kwa kima cha pauni mil 75.

No comments