WENGER AKUTANA NA MBAPPE KUMSHAWISHI ATUE LONDON

VYOMBO vya habari nchini Ufaransa vimefichua kuwa kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alikutana na mshambuliaji kinda wa klabu ya Monaco, Kylian Mbappe ili kumshawishi atue London.

Wenger anamtaka mshambuliaji huyo ili kuziba pengo la Sanchez ambaye yuko mbioni kukikacha kikosi hicho katika kipindi hiki cha usajili.


Hata hivyo, kuna uwezekano mdogo kwa Wenger kumnasa Mbappe baada ya Real Madrid kuwemo kwenye vita hiyo.

No comments