WENGER ASEMA LACAZETTE ANA MAMBO YOTE ALIYONAYO SANCHES NA PENGINE KUMZIDI

KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa muuaji wa makipa, Alexandre Lacazette ana mambo yote ambayo Alexis Sanchez anayo na pengine kumzidi, ingawa hana maana kwamba Sanchez ni mshambuliaji mbaya.

Habari mpya ni kwamba nyota huyo anaweza kutua katika klabu hiyo wakati wowote kwa sababu klabu yake ya sasa imetoa baraka zote.

Kocha wa kikosi hicho, Arsene Wenger amesema kwamba amehakikishiwa na mtu mmoja muhimu kwamba anaweza kumpata nyota huyo wakati wowote.

Na hii maana yake ni kwamba, arsenal sasa inaweza kuamua kuachana kabisa kiroho safi na “msumbufu” Alexis Sanchez, mtu ambaye ameifungia klabu hiyo mabao 30 katika mashindano yote.

“Nimehakikishiwa na rais wa Lyon kwamba Lacazette ni mchezaji tunaeweza kumnasa wakati wowote,” amesema Wenger.

“Katika kipindi hiki ambacho Sanchez anaondoka na Danny Welbeck ni majeruhi, tunatakiwa kuwa na Arsenal yenye watu ambao watatuhakikishia mabao mengi,” amesema.

“Tunatakiwa kuwa na washambuliaji wenye uhakika wa kupigania timu. Ni wakati wa kuwa na washambuliaji wakali zaidi,” amesema Wenger.

Katika mabao 37 aliyofunga Lacazette, anaonekana kama ni mtu mwenye uhakika wa kufanya makubwa zaidi akiwa na Arsenal.

Arsenal ina wasiwasi mkubwa wa kuwakosa nyota wengi na hasa ikizingatiwa kuwa kikosi chake kina orodha kubwa ya wachezaji majeruhi, lakini pia Olivier Giroud anayetajwa kama roho ya timu nae anataka kuhamia Lyon.

Lakini hatua ya rais wa Lyon, Jean-Michel Aulas kuihakikishia Arsenal kwamba wanaweza kumpata Lacazette, inaonyesha wazi kwamba sasa Parc Olimpique Lyonnais hawana chao.


“Alexandre anaweza kuondoka Atletico, lakini hawezi kuondoka katika timu ambayo ina malengo mengi. Hapo ndipo unapoona kwamba wakati huu kila mchezaji anatakiwa kufanya tafakuri kubwa,” amesema Aulas akihojiwa na shirika la habari la AFP.

No comments