WENGER SASA AMTOLEA MACHO KINDA WA MIAKA 19 KUTOKA UJERUMANI

KAMA kuna mtu anajua hesabu za kusajili, basi huyo ni kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye pamoja na kulalamikiwa sana na mashabiki wake lakini linapokuja suala la usajili anakuwa makini sana.

Wenger baada ya kufanikisha dili la usajili wa Alexander Lacazette sasa amemtolea macho kiungo wa Eintracht, Frankfurt ya Ujerumani, Aymen Barkok kinda ambaye ana umri wa miaka 19 tu.

Mtandao wa Spox umeandika kuwa usajili wa nyota huyo kwenda Arsenal unaweza kukamilika muda mfupi ujao na hilo kwa Wenger sio tatizo.

Wenger anataka kuhakikishab kwamba katika kipindi hiki cha usajili anawauza baadhi ya wachezaji ambao wanatakiwa na klabu nyingine ili aweze kupata fedha za usajili wa nyota anaowataka.

Habari mpya ni kwamba Marseille ya Ufaransa wanaongoza katika mbio za kumsajili Olivier Giroud ambaye sasa ana miaka 30 kwa kitita cha pauni mil 24.7.


Lakini kituko ni kwamba Arsenal hawataki kulipa kiasi ambacho Leicestar wanakitaka ili kumsajili winga Riyad Mahrez mwenye umri wa miaka 29, ambaye anatarajiwa kuondoka Leicester msimu huu.

No comments