WESTHAM UNITED, TOTTENHAM ZAINGIA VITANI KUWANIA SAINI YA KIUNGO WA ZAMANI WA CRYSTAL PALACE

KIUNGO wa zamani wa Crystal Palace, Mathieu Flamini amezingiiza katika vita ya kumwania timu za Westham United na Tottenham Hotsur.

Hii ni baada ya Flamini kumaliza kandarasi yake ndani ya Crystal Palace na sasa anakuwa mchezaji huru baada ya kuitumikia timu hiyo kwa mafanikio.

Flamini ambaye mkataba wake ndani ya Crystal Palace ulifikia tamati Julai mosi, mwaka huu, ameanza kupokea ofa za uhamisho kutoka timu mbalimbali za ndani na nje ya England.

Timu za Westham na Tottenham zimeingia katika mbio za kuwania saini ya nyota huyo.

Ingawa kwa sasa hajaamua hatma yake, lakini kuna taarifa kuwa Flamini ana nafasi ya kusajiliwa kama mchezaji huru ifikapo katikati ya msimu wa usajili wa dirisha la sasa la majira ya kiangazi.

Akinukuliwa, Flamini aliweka bayana kuwa amepokea ofa kutoka klabu mbalimbali barani Ulaya pamoja na timu za nchini China, Japan na Uturuki.


Hata hivyo, mwenyewe amesema anahitaji kucheza soka katika Ligi iliyo na ushindani na sasa yumo katika kupembua ipi timu anayodhani atajiunga nayo ingawa mazungumzo bado yanaendelea.

No comments