YAH TMK MODERN TAARAB KUIPASUA IFAKARA JULAI 28 …Julai 29 ni Kilosa, Julai 30 Dumila


Kundi zima la Yah TMK Modern Taarab, linatarajiwa kuuteka mji wa Ifakara Julai 28 kwa burudani itakayomininwa ndani ya ukumbi wa Jamos.

Waandaji wa onyesho hilo – Jamos Entertainment, wameiambia Saluti5 kuwa kundi hilo linasubiriwa kwa hamu kubwa na wakazi wa Ifakara.

Miongoni mwa wasanii wanaotarajiwa kuiteka Ifakara ni pamoja na Omar Teggo, Fatma Mcharuko, Aisha Vuvuzela, Muawa Teggo, Mohamed Mauji na Chid Boy.

Mbali na show ya Ifakara, Yah TMK  watatumbuiza Kilosa Julai 29 ndani ya ukumbi wa Babylon Luxury Pub kabla ya kuelekea Dumila Julai 30 kwenye ukumbi wa Dumila Pub.

No comments