YANGA MAZOEZINI "SHAMBA LA BIBI" UWANJA WA TAIFA MUDA HUU

KIKOSI kamili cha Yanga muda huu muda huu kimeanza kuingiza gia ya pili ya mazoezi yake ambapo kimehamia rasmi uwanjani ambapo vifaa vipya vinaanza kuonyesha ufundi wao mbele ya makocha wao.

Yanga chini ya kocha George Lwandamina imetumia wiki moja kujifua katika gym ambapo huko walikuwa wakifanya mazoezi mazito ya kujaza nguvu mwili chini ya wataalam waliobobea ambao waliwafanyisha mazoezi mazito wachezaji wa timu hiyo.

Baada ya ratiba hiyo ya gym, leo kikosi hicho kitakuwa na sehemu mbili za mazoezi ikiwa ni ongezeko la mazoezi hayo kutoka kwa Lwandamina ambaye amepania kuisuka Yanga ngumu katika kufungwa, lakini ikiwa na makali ya kumfunga yoyote.

Ratiba hiyo inaonyesha kwamba Yanga itakuwa na mazoezi ya mwisho ya gym kisha jioni kubadili gia na kuingia uwanjani kuanza kuangalia ufundi wa wachezaji wake katika mazoezi ambayo yanasubiriwa na wengi.

Katika hatua hiyo ya mazoezi ya uwanjani, vifaa vipya vilivyosajiliwa kama washambuliaji Ibrahim Ajib, Pius Buswita, kiungo Fenando Bongnyang na beki Henry Okoh Tony raia wa Nigeria wanaojaribiwa, wataonyesha hadharani uwezo walionao uwanjani.


Bongnyang raia wa Cameroon ambaye tayari ameanza kuwateka makocha kwa uwezo wake wa kumudu mazoezi makali, atakuwa na wiki moja ya uwanjani kuweza kuthibitisha ubora wake pamoja na Okoh Tony endapo wataweza kuwashawishi watapewa mikataba ya miaka miwili kila mmoja.

No comments